Mwarabu Fighter Azungumzia Kuhusu Kumlinda Irene Uwoya.

aliyewahi kuwa mlinzi wa msanii Diamond Platinumz amefunguka na kuongelea swala la yeye kwa sasa kuwa karibu na kuonekana karibia kila mahalia kiwa na mwanadada Irene Uwoya , na kusema kwa sasa amekuwa akifanya kazi na msanii huyo.

Mwarabu Fighter ambae baada ya kuacha kufanya kazi na Diamond alifungua kampuni yake ya ulinzi na kusema kuwa kwa sasa anafanya kazi na mtu yoyote hata kwa masaa kulingana na vile wanavyolipwa.

download latest music    

Mwarab Fighter anasema kuwa mwanadada huyo ndio aliemtafuta na kuataka huduma kutoka kwake.

Akizungumza na Wasafi Tv, Mwarab fighter anasema “Irene kwa mara ya kwanza aliponihitaji alikuja ofizini kwangu na sio kwamba niko nae kila anapokwenda.mimi ninamheshimu tu kama mtu anayeniletea riziki na siwezi kumchunguza hayo mambo yake mengine.”

Mwarabu Fighter kwa sasa anamiliki kampuni ya ulinzi na imekuwa ikifanya kazi na mtu yoyote kwa muda wote kulingana na makibaliano na malipo kati ya kampuni na mteja.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.