Mwasiti Adai Umri Hauwezi Kumkatisha Tamaa Ya Kufanya Muziki

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Mwasiti Almasi amefunguka na kuweka wazi kuwa hawezi akaacha kufanya Muziki kisa eti anahofia umri unakuwa unamtupa mkono.

Mwasiti amefunguka na kudai umri wake hauwezi kuwa kikwazo kwake binafsi kwani anaamini bado ana uwezo mkubwa sana wa kufanya kazi nzuri ambazo zikavutia mashabiki zake.

download latest music    

Kwenye mahojiano na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa radio, Mwasiti amefunguka:

Sijawahi kukata tamaa na muziki bado nina uwezo wa kufanya. Toka nimeanza muziki naweza kusema nimetimiza asilimia 60 ya malengo yangu. Umri sio tatizo katika kufanya kazi maana hata ukimuangalia Joseph Haule ‘Profesa Jay ni mbunge lakini still anaendelea kupiga kazi”.

Hata nje ya nchi kuna  wasanii wenye umri mkubwa lakini huwasikii wameacha kufanya Muziki, licha ya kuwa kuna umri ukifika huwezi kuonekana kwenye majukwaa ukifabya shoo”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.