Mzee Majuto aeleza vitu ambazo atajishugulisha nazo baada ya kuamua kustaafu

Alhaji Amri Athumani maarufu kama Mzee Majuto sasa ameamua kuachana na mamba ya sanaa baada ya kufanya kazi ya uigizaji kwa takriban miaka 30.

Mwezi jana muigizaji huyo mkongwe aligonga vichwa vya habari baada ya taarifa potovu kuidai kuwa ameaga dunia ghafla nyumbani kwake Tanga.

download latest music    

Mzee Majuto sasa ameeleza kuwa ameamua kustaafu baada ya kuona umri wake unaenda na uwingi wa changamoto wa kazi yake ya uigizaji.

kwenye mahojiano yake na gazeti la Habari Leo, muigizaji huyo alifunguka na kusema kuwa yeye sasa atajishugulisha na kilimo na kumtumikia Mungu.

“Kwa sasa hivi mimi sanaa basi , nasema kwa kweli sanaa basi labda kutokee mtu anahitaji nimfanyie tangazo lake nikimaliza narudi shambani kwangu nimtumikie mwenyezi Mungu nimuombe toba kwa sababu tuliofanya ni mengi na kuna mazuri na mabaya na mabaya ndiyo yanayotawala kwenye maisha ya ujana kwa hiyo tumuombe toka Mwenyezi Mungu, kwani wakati ndiyo huu ukisema upange siku kila siku utapanga,” Mzee Majuto alisema.

Tazama mahojiano hayo hapo chini:

https://youtu.be/Sf9_vue0ttc

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere