Mzee Majuto Akiri Sinema Kuwa Ndio Kila Kitu Kwake.

Msanii mkongwe na maigizo na vichekesho nchi Mzee Majuto  ambae amekuwa ni kama mlezi kwa wasanii wengine wa bongo movies amekiri kuwa kazi za sinema na filamu ndio kila kitu katika maisha yake na ndio zinazompa kula na kuishi mjini kwa miaka yote.

Akiongea na wasanii wenzake Jb na Single Mtambalike hivi karibuni walipomtembelea hospitali ambapo amelazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu, Mzee Majuto anasema kuwa anaishukuru na kuheshimu kazi hiyo kwa sababu ndio iliyompa kula na kuishi mjini, huku kisema kuwa pamoja na kwamba amekuwa mgonjwa kitandani lakini ndani anakazi  nane ambazo hazijatoka huku akiitaja ya uganga ndio iliyotoka tu.

download latest music    

Nina miaka 70 sasa na kazi kubwa inayoniweka mjini ni hii ya sinema,nina movis nane nimeziweka ndani kwaio sina presha.nikisikia njaa natoa moja nauza napata kula. na katika hizo nane nimeuza moja tu ya uganga basi.-Alifunguka Mzee Majuto.

Mzee Majuto yuo katika hospitali ya Tumaini jijini Dar, ambapo alilazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya upasuaji wa tezi dume iliyokuwa ikimsumbua kwa muda mrefu, hata hivyo hali yake inasemekana kuimarika .

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.