Mzee Majuto Bado Mgonjwa,Tumuombee:- Mke wa Majuto Awaomba Mashabiki

Mke wa mchekeshaji maarufu nchini Mzee Majuto anaejulikana kama Aisha  Yusuf ameowaomba wasanii, na mashabiki wake kwa ujumla kumuombea sana mzee majuto kutokana na hali yake kuwa mbaya kwa sasa baada ya kufanyiwa upasuaji na kidonda kushindwa kupona.

Hata hivyo aisha ansema kuwa mzee majuto alifikishwa hospitali hapo akiwa na hali mbaya sana wikiendi hii lakini anashukuru mungu kwa sababu kidogo hali yake imebadilika na kuwa nzuri.

download latest music    

Ninachowaomba tu watanzania, wamuombee mume wangu ili aweze kupona na pia tutoke hospitali kwa sababu akilala na mambo yote yanalala.

Mke wa Majuto anasema kuwa mzee majuto amefanyiwa upasuaji wa mara ya pili wa henia baada ya kuwa wanatafuta tiba ya ugonjwa mwinhine na ndipo walipogundua tatizo hili la tezi dume , walipomfanyia mwaka huu januari lakini kidonda bado kinasumbua kupona.

Wakati tunahangaika kupata matibabu ya nyoga ndipo alipogundulika kuwa anatezi dume ndipo alipofanyiwa upasuaji.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.