Loading...

Mzungu Wa Nisha Anadaiwa Kuwa Mume wa Mtu na Familia Yake

July 11, 2018 at 09:42
Mzungu Wa Nisha Anadaiwa Kuwa Mume wa Mtu na Familia Yake
Loading...

Msanii wa filamu za Kibongo aliyegeukia na Bongo fleva Nisha Bebe amedaiwa kuwa amemchukua mume wa mtu na kisha kumtambulisha kama mpenzi wake.

Siku mbili hizi Nisha ametengeneza sana headlines Kwenye mitandao ya kijamii baada kurusha picha na video zilizomuonyesha akiwa na mzungu ambaye amemtangaza kama mpenzi wake.

Loading...

Lakini mara moja taarifa zimeenea kuwa mzungu yule hana uhusiano na Nisha kwani ni mume wa mtu na ana Familia yake na watoto na mwanamke mwingine ambaye picha zake zimesambaa Mtandaoni.

Hizi ni baadhi ya picha zinazomuonyesha mzungu wa Nisha akiwa na mwanamke anayesemekana kuwa ni mke wake:

 

 

 

Baada ya Tetesi hizo kusambaa kuwa Nisha kumuona mume wa mtu na kuharibu familia ya watu alifunguka na kukataa tuhuma hizo ambapo alisema:

Walimwengu huwezi kuwakataza kuongea, kama wana ushahidi wa vyeti vyake vya ndoa waniletee“.

Nisha pia amekataa taarifa kwamba huna uhusiano na mwanaume huyo bali ni kiki tu ya ngoma yake mpya ambayo anategemea kuitoa hivi karibuni.

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…