“Nagombana Sana na Rayvanny Ila Ndio Nishampenda Simuachia”- Fahyma

Mpenzi na Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Rayvanny, Fahyma au Fahyvanny amefunguka na kuweka wazi Siri ya kudumu kwenye Penzi kwa muda mrefu.

Tofauti na mastaa wengi Rayvanny na Fahyma ndio kapo ya WCB ambayo imedumu kwa muda mrefu na hii ni tangu walipoanzisha mahusiano miaka michache iliyopita Baada ya kukutana kwenye moja ya video za Rayvanny ambapo Fahyma alikuwa video queen.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Amani, Fahyma alisema kwamba, watu wengi huwa wanahisi yeye na mzazi mwenzake hawagombani kitu ambacho si kweli, huwa wanagombana mara nyingi ila upendo na uvumilivu ndivyo vinawafanya waendelee kudumu mpaka sasa.

Kuna watu huwa wanafikiri mimi na mzazi mwenzangu hatugombani, kitu ambacho si kweli huwa tunagombana sana tu, ila sema binafsi nilishaamua kutulia naye, nampenda basi inatosha na ndiyo maana hamjawahi kusikia nina bwana mwingine zaidi yake“.

Rayvanny alishatangaza ndoa na Fahyma na hata kumpeleka kumtambulisha nyumbani kwani Mbeya mwaka jana.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.