Najua Tabia Za Diamond Nikiwa Naye Atanisumbua Sana- Wema Sepetu

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu kwa mara nyingine amejibu tetesi zilizozagaa kuwa amerudiana na aliyekuwa mpenzi wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Tetesi za Wema kurudiana na Diamond zilianza kuapmba moto Miezi michache iliyopita baada ya Zari kutangaza kuwa alimuacha Diamond baada ya kumuona amekumbatiana na Wema huku akidai wamerudiana Tena.

download latest music    

Lakini Wema siku zote amekuwa akikataa tetesi hizo na kusisitiza kuwa Diamond ni rafiki yake wa karibu tu. Lakini Siku mbili hizi imedaiwa Wema alibeba ujauzito wa Diamond jambo ambalo amelikataa na kusema tayari ana mpenzi wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Wema ameweka wazi kuwa hawezi kurudiana na Diamond kwani anajua tabia zake lakini pia amesema hata akitaka kumuoa hawezi kukubali:

Yaani Diamond, hata aache kila kitu akaniambia sasa Wema nataka kukuoa sitakubali kabisa Alafu nilimpenda zamani, lakini siyo sasa kwa sababu Nasibu nimekaa naye miaka miwili. Najua alivyo na hatanisumbua sana kwa sababu mimi nilimwacha CK kwa ajili yake, matokeo yake akatoka na Meninah (msanii wa Bongo Fleva) na meseji nilizibamba. Kwa hiyo hata kwenye ndoa hawezi kubadilika.

Lakini pia Wema amejitetea kuhusu suala la yeye kuonekana anaenda nyumbani kwa Diamond Madale ni jambo la kawaida kwani alienda kwenye swimming party aliulizwa tu na Diamond kama rafiki yake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.