“Nampenda sana Ben Pol” afunguka Ebitoke

Bado akiwa katika umri mdogo na mgeni katika tasnia hii ya uchekeshaji  lakini amejitwalia umaarufu mkubwa ,mchekeshaji huyu   wa kike chipukizi Anna exavery anayejulikana  maarufu kama Ebitoke ameongelea muendelezo ya ukaribu wake na msanii wa muziki wa kizazi kipya Ben pol  na kusema kuwa bado  anampenda sana ben pol na amekuwa akisikia wivu sana anaposikia watu katika mitandao  wanasema kuwa ben pol ana wanawake wengine  wakati yeye lengo lake kubwa ni kujenga mahusiano mazuri na ben pol na hatimaye baadae  kufunga ndoa  na kuwa na  familia pamoja kwa uwezo wa mwenyezi mungu.

“lengo langu lipo pale pale   ni kumuomba Mungu  anisaidie nije kuolewa na Ben pol ,nampenda sana  naamini mambo yataenda vizuri na mipango’ anasema mchekeshaji huyo, akiongelea pia kuhusu swala ya yeye kuwa bado bikra E bitoke anasema kuwa  swala ilo huwa hapendi kuliongelea sana maana alishaliongea tayari kwa muda . hata hivyo tukirudi nyuma kidogo katika kulizungumzia swala hili msanii ben pol pia alipoulizwa katika usiku wa fiesta pale mkoani Arusha alikaririwa akisema kuwa ‘ Tuko karibu ,ni mtu poa mtu mzima anajiamini na ana malengo hivyo atafika mbali’ alipoulizwa kuhusu mahusiano yake na ebitoke kwa sasa  Ben pol alikataa kuongelea swala ilo kwa kudai kuwa wataaribu vibes za fiesta ivyo hawezi kuongelea swala hilo.

download latest music    

Kumekuwa na picha tofauti tofauti zinaowaonyesha wawili hao wakiwa pamoja sehemu mbalimbali ,ben pol amekuwa akisema yeye na ebitoke ni watani na  marafiki tu  na amekuwa nae karibu kwa sababu amemuomba  ili kumsaidia katika kutangaza kazi zake za kiusanii huko ebitoke akionekana kuwa serious na mahusiano .hata hivyo bado ni jamboi zuri kwa msanii mkubwa kama ben pol anapokua ameona kipaji cha msanii na mchekeshaji huyo na kukubali kufanya nae kazi ilik kuweza kumuinua katika kazi zake hii inaonyesha ni jinsi gani ambavyo wasanii wakubwa wapo tayari katika kusaidia wale ambao ndio wanachipukia katika game

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.