Nandy Adaiwa Kumnyakua Bwana Wa Wema

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Aibu’ Faustina Charles maarufu Kama Nandy amedaiwa kumchukua Mwanaume aliyekuwa kwenye mahusiano na muigizaji Wema Sepetu.

Gazeti la Risasi linaripoti kuwa Mwanaume mmoja anayejulikna Kama Rajabu ambaye ni mfanyabiashara wa Mwanza alikuwa ndio anamuweka Wema mjini lakini Baada ya skendo ya Wema na PCK kutokea inadaiwa bwana huyo alimtosa Wema na kuhamisha majeshi kwa Nandy.

download latest music    

Gazeti hilo linaendelea kuripoti kuwa mara tu baada ya mwanaume huyo kutua kwa Nandy alimpangishia nyumba Masaki jijini Dar na kumnunulia gari la kifahari aina ya BMW X 1 na pia siku ya birthday yake mwanaume alimwagia pesa chafu ukumbini.

https://www.instagram.com/p/Bp9dZByBMxh/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=pqpdgwd4nx78

Baada ya tetesi hizo Gazeti hilo lilimsaka Nandy ili kupata ukweli wake juu ya ishu ambapo alikana kabisa taarifa hizo na kukana kumjua jamaa huyo.

Mh! Waja wana mambo sana, kwanza niseme nashtuka wewe kuniambia mambo ya bwana wa Wema, mimi yule bwana alinipa kama milioni tano hivi nilipozihesabu na nilishangaa kwani sikuwa nikijua kuwa nitapewa pesa hizo lakini si mpenzi wangu, wala sijawahi kujua kama anatoka na Wema.

Ukweli ni kwamba nilimualika kwenye pati yangu akanipa pesa kama mlivyoona lakini sina uhusiano naye wa kimapenzi na wala gari hili hajaninunulia yeye, mimi nimejinunulia mwenyewe kwa kazi zangu tu. Kuhusu nyumba nimepangishiwa na mpenzi wangu ambaye siwezi kumtaja kwa sasa ila ni mtu maarufu tu.

Lakini Nandy alipobanwa zaidi kuhusu jamaa huyo alisema:

Alinipigia simu na kuniambia kuwa anataka kufanya biashara na mimi, akaniambia atakuja Dar, huwezi kuamini alikuja Dar na ikawa ndio imefika siku ya sherehe yangu ya kuzaliwa, nikamualika kwa bahati nzuri akaja”.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.