Napenda Mwanamke Anayejiamini- Ben Pol

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Bernad Paulo maarufu kama Ben Pol amefunguka kuhusu aina ya mwanamke anayempenda. Mwana muziki huyo amekuwa katika vichwa vya habari sana kutokana na kutajwa na mchekeshaji maarufu Anastazia Kisaveli ‘Ebitoke’.

Ebitoke amemtaja mara kwa mara kwamba anampenda kimapenzi Ben Pol lakini kijana huyo amepotezea. Katika mahojiano yake aliyoyafanya hivi karibuni Ben Pol aliweka wazi kuwa hana muda wa kumuongelea Ebitoke kwani kulitokea mvurugano baada ya Meneja wa Ebitoke kutoka Timamu tv kudai kuwa alimlipa Ben Pol kiasi cha shilingi milioni tatu ili tu aonekane na Ebitoke katika mitandao ya kijamii lakini Ben Pol amekataa tuhuma hizo.

download latest music    

Ben Pol ameweka wazi kuwa kitu pekee anachoangalia kwa mwanamke ili awe naye kimapenzi ni lazima awe najiamini pindi wanapokuwa kwenye maongezi.

“Endapo nikimpenda msichana kitu kikubwa ninachoangalia ni ‘confidence’ yake hasa pindi tukiwa tunachat, usmart, umakini na uharaka wa kujibu vitu unavyokuwa unaulizwa kwa wakati huo”.

Ben Pol ni moja kati ya wanamuzi wanaopendwa sana na wadada yaani mashabiki wake wengi ni wasichana kutokana na aina ya muziki anayoimba hata pia na muonekano wake . Hivi sasa Ben Pol anatamba na nyimbo yake mpya inayoitwa kidume aliyomshirikisha mwanamuziki kutoka Nigeria inayofanya vizuri sana katika stesheni nyingi za redio nchini.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.