Natukanwa Nikimpost Hamisa:-Esha Buheti

Mwanadada Esha buheti kutoka bongo movies amefunguka na kusema kuwa mashabiki zake wamekuwa wakimtukana kila anapopost baadhi ya mastaa katika page yake kutokana na teams zilizopo katika mitandao ya kijamii.

Hata hivyo Esha anasema hawezi kuacha kumposti kwa sababu wao hawana ugomvi wowote na pia wamekuwa wakisapotiana sana ktika kazi zao hivyo hawezi kusikiliza kila mtu.

download latest music    

Lakini pia Esha Buheti anasema kuwa pamoja na kwamba yeye ni team kiba lakini biashara zake haziingiliani na u-team na ndio maana hata chakulaanachopika anapewa sapoti sana na kina esma platinumz, mama dangote na hata Petiti man ambae ni mume wa Esma ambao hao wote ni familia ya Diamond.

Hamisa  ni mdogo wangu, ninatukamwa sana ninapompost hamisa, esma ni mteja wangu mkubwa wa chakula pia mama dangote,karibia nusu ya Ramadhani yote Esma, Petit walikuwa wateja wangu sana.

Hata hivyo Esha anasema kuwa yeye yupo kwa ajili ya kumsapoti alikiba na hata wakati anataka kwenda kwenye mpira alimuuliza kuhusu hilo na alimjibu ni kweli ameamua kucheza mpira wakaongea na kucheka tu.

Kwa upande mwingine, Esha anasema kuwa wakati wapo katika harusi ya zabibu alisikia watu walikuwa wakisema kuwa msanii huyo kwa sasa ni kama anaumwa kwa sababu sauti yake inakuwa inakuja na kupotea.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.