Ndoa 5 Za Mastaa Zilizo-kiki Kwa Mwaka 2017

December 15, 2017 at 07:34
Ndoa 5 Za Mastaa Zilizo-kiki Kwa Mwaka 2017

Mwaka 2017 umekuwa mwaka wa kila jambo na matukio mbali mbali kwa mastaa wetu wa Bongo mojawapo kati ya matukio yaliyochukua nafasi ya kutrend sana ni ndoa za mastaa mbali mbali.

Ndoa zilizo fungwa na mastaa mbali mbali zilitawala nakushika headlines na leo tutaangalia Ndoa tano za mastaa zilizotrend sana mitandaoni na hata mitaani ambazo kila mtu alikuwa anaziongelea.

Loading...

1. Shilole na Uchebe

Ndoa ya Shilole na Uchebe ilikuwa ndoa yenye utata sana ambao ulianzia kwenye familia kwani habari zinadai kuwa familia ya Shiloke haikutaka aolewe na Uchebe hadi kufikia hatua ya kupelekana polisi na hadi siku ya harusi ilifanywa kwa siri na kuhudhuriwa na watu kumi.

2. Rommy Jones na Kay Jord

Ndoa hii ilikiki kwa staili ya kipekee kwani bwana harusi ni kaka Wa mwanamuziki maarufu Diamond Platnumz kilichowavutia watu wengi ni Diamond na Zari kuwa wasimamizi lakini pia familia ya Diamond kutoa zawadi za mamilioni kwa maharusi.

3.Ndoa Ya  Proffesor Jay

Ndoa ya mbunfe wa Mikumi Proffesor Jay iliwavutiwa watu wengi keani ni harusi iliyowakutanisha Wasanii wakongwe wanasiasa na watu mbali mbali lakini pia ndoa hiyo ilisindikizwa na sherehe tatu.

4. Joti na Tumaini

Harusi ya Joti ilizungumziwa sana kwanza kwa sababu hakuna mtu aliyeamini Kama kweli anafunga ndoa watu wengi walijua ni utani tu au litakuwa tangazo lakini ilikuwa ni ndoa kweli na ilikiki sana.

5. Irene Uwoya na Dogo Janja

Hii ndio ndoa ambayo inaweza ikawa imefunika mwaka 2017 kwani ndoa hii ilizungumziwa sana kupita kiasi yote ikisababishwa na tofauti ya umri wa Dogo Janja na mrembo Uwoya.

 

Leave a Reply

avatar

in Entertainment
Loading...

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.