Ndoa ya Ali Kiba Yamtoa Dully Sykes Mapovu

April 16, 2018 at 15:55
Ndoa ya Ali Kiba Yamtoa Dully Sykes Mapovu

Msanii mkongwe wa kizazi kipya Dully Sykes amefunguka na kutoa yaliyo moyoni mwake kuhusu kutokualikwa katika harusi ya msani Alikiba inayotarajiwa kufungwa mwishoni mwa wiki hii huko Mombasa Kenya.Dully analalamika kutokana na ukweli kwamba taarifa hzio amekuwa akiziona katika mitandao wakati yeye ni moja kati ya watu muhimu sana katia mafanikio ya muziki wa Alikiba.

Dully anasema kuwa yeye ni moja ya watu waliotambua kipaji cha alikiba kipindi ambacho hata alikuwa hajulikani  na kwamba alijitahidi hata kumtoa katika muziki lakini anashangaa kuona anapata taarifa katika mitandao na kupigiwa simu na watu kutoka kenya kumwambia kuhusu taarifa hizo bila kupewa taarifa na muhusika.

Loading...

mimi hajaniambia chochote zaidi ya kuonakatika mitandao ya kijamii na kupigiwa simu na dada yangu kutoka kenya kuwa alikiba anakuja kuoa kenya,lakini alikiba hajaniambia chochote wakati mimi ndie nilikuwa mtu wa kwanza kumuamini alikiba na kumsapoti  kipindi hicho hakuna hata mtu aliyekuwa anamjua alikiba hata nyumba ya jirani walikuwa hawajui kama kuna msanii  na niliposikia sauti yake tu nilimuomba kolabo-Alizungumza Dully alipokuwa akiongea na Big chawa.

Dully anasema kuwa hata kama hajaalikwa lakini bado anamped sana alikiba na amekuwa akimpenda siku zote na anamtakia maisha maema na mafanikio katika ndoa hiyo na kumsihi kumpenda na kumheshimu mwanamke anaekwenda kumuona na kumpedna sana ukizingatia ni mtu kutoka nchi jirani.

Namtakia ndoa njema na nampenda sana na anajua hilo, namtakia maisha mema ya ndoa na namsihi sana ndoa sio kitu kidogo maana anapoamua kuchukua mtoto wa watu tena hasa kutoka nchi nyingine  inabidi amuheshimu sana na kumpenda sana ili ata binti wa watu anapoitwa na wazazi wake kwanini huji kutusalimia hakose cha kujibu kwa sababu ya upendo.

Leave a Reply

avatar

in Entertainment
Loading...

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.