Ndoa ya Sasha Yavunjika ,Ni Baada ya Kukatazwa Kutumia Mitandao

January 12, 2018 at 13:07
Ndoa ya Sasha Yavunjika ,Ni Baada ya Kukatazwa Kutumia Mitandao

Ile ndoa ya msanii Sasha Khassim iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na msanii huyo imevunjika na haitafanyika tena kama awali ilivyokuwa imetangazwa na mwanadada huyo.sasha amesema kuwa kama kuna watu walikuwa wakisubiria ndoa hiyo basi wajue kuwa haipo tena na hata mahali haitarudishwa.

Akizungumza na GPL, Sasha amesema kuwa mwanaume huyo alijulikana kwa jina la Boniphace, wameshindwa kumudu nae katika  mapenzi na ameona kuwa hawzi kuwa nae kwa sababu ya wivu wake.sasha anasema kuwa mwanaume huyo amekuwa akikasirika sana kila anapokuta ameposti picha katika mitandao ya kijamii na kufikia hatua ya kumwambia kuwa aachane na mitandao ya kijamii kitu amcacho yeye hawezi kwa sababu hata yeye alimpata kupitia mitandao ya kijamii.

Loading...

sasha anasema kuwa hayuko tayari kuacha kuweka picha katika mitandao ya kijamii hivyo ni bora aachane na mwanaume huyo.suala la ndoa halipo tena,yeye alinipa katika mitandao ya kijamii lakini cha ajabu ananikataza kabisa kutumia mitandoa ya kijamii.nimeona sitaweza kujinyima uhuru  wa maisha yangu kiasi hiki, hivyo uchumba umevunjika na mpango wa kurudisha mahali haupo kabisa.  -Alifunguka Sasha.

Mwanadada huyo amekuwa akijitapa kwa muda mrefu kuwa  ataolewa na mwanaume kutoa nje ya nchi na atakuwa akifanyakazi zake nchini na kurudi nje kwa mumewe lakini ndoto hizo zimevunjika baada ya kushindwa kuweka mambo sawa.

5
Leave a Reply

avatar
5 Comment threads
0 Thread replies
0 Followers
 
Most reacted comment
Hottest comment thread
1 Comment authors
FaridaGladysMariamJacobIBRAHIM Recent comment authors
newest oldest most voted
IBRAHIM
Guest
IBRAHIM

Heri ndoa ivunjike upuzi mtupu

Jacob
Guest
Jacob

Namshangaa sana sasa kupost atanufaika na nini?

Mariam
Guest
Mariam

Hana akili kabisa

Gladys
Guest
Gladys

Ala? imefikia hapo?

Farida
Guest
Farida

Akili za kitoto sio nzuri


in Entertainment
Loading...

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.