Ndoa Ya Zamaradi Yageuka Gumzo Mitandaoni

Akiwa ni mmoja wa wanadada wanaopendwa na watu wengi katika mtandao kutokana na ushauri na maneno yake anayopost katika ukurasa wake wa instagram na katika kipindi chake, mwanadada mrembo Zamaradi Mketema ambae ni mwanzilishi na mwendeshaji kipindi cha ‘Take One’ , kinachorushwa na Clouds Tv  amefunga ndoa Ijumaa iliyopita na mwanaume anaesadikika kuwa ni mtoto wa kigogo.

Ndoa iyo ambayo imeshangaza watu kidogo na kuwa tofauti na ndoa nyingine,  mwanadada huyo aliamua kufungwa ndoa  kimya kimya, kilichoonyesha ndoa imefungwa ni picha zilizoanza kusambaaa mitandao mara baada ya ndoa kufungwa.Akiwa kama mtu maarufu na anaependwa na watu wengi, mashabiki na watu wanamwangalia walitarajia ndoa isingekuwa ya kimya kimya, hata hivyo ndoa hiyo ya Zamaradi amefunga na mwanaume ambae si kama wengi walivyotarajia kutokana na kuwa wengi walimjua mwanaume mwingine tofauti na aliyefunga nae ndoa.

download latest music    

Huku wengi wakimpongeza zamaradi ambae inasemekana aliachana na mwanaume ambae ni baba wa watoto wake wawili lakini  pia ni bosi wake na mtu maarufu anaejulikana kama Ruge Mutahaba ambae ni mkurugenzi wa uzalishaji wa vipindi Clouds Media.Kwa muda mrefu imekuwa ikijulikana kuwa Zamaradi ana mahusiano ya kimapenzi na bosi uyo hivyo swala la Zamaradi kuolewa na mwanaume mpya tofauti na yule kidogo imeleata utata katika mitandao.

Hata hivyo , alipokea pongezi nyingi kutoka kwa watu mbalimbali, ilhali wengine wakionekana kumsifia kitendo chake cha ujasiri cha kuachana na baba mzazi  wa watoto wake.iInaonekana kuna vitu vingi chini ya carpet vinavyohusu ndoa hiyo, huku wengine wakijaribu kufanya uchunguzi wa kina kuhusu ukweli wa mwanaume wake ambae pia ameleta utata wa kazi yake na umaarufu wake mjini.Wapo wanaosema kuwa ni ndugu wa kigogo mkubwa nchini , huku wengine wakisema kuwa ni moja wa misheni town wa mjini.Hata hivy Zamaradi mwenyewe pia alithibitishao ukweli wa ndoa hiy katika ukurasa wake kwa kusema “Inshallah , na Iwe kheri”

Wasanii wengine waliompongeza Zamaradi ni pamoja na Faiza Ally, Jackiline Wolper,  na Batuli.Ikiwa ndoa ni jambo la kheri na ndoto ya watu wengi basi tunamtakia kheri na baraka katika ndoa yake mwanadada Zamaradi Mketema.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.