Ndugu Wamwaga Povu Siku 7 Baada Ya Ndoa Ben Kinyaiya

Ikiwa  zimepita siku chache tangu Mtangazaji mkongwe Ben Kinyaiya Afungukia ndoa ambayo ilizua gumzo kwenye Mitandao ya kijami, mapya yameibuka kuhusu sakata hilo huku familia ikihusishwa.

Gazeti la Risasi Jumamosi linaripoti kuwa Ben Kinyaiya amejikuta akicharukiwa na ndugu wa mwanamke kwa kushindwa kumtetea ubavu wake huyo.

download latest music    

Kwa mujibu wa mmoja wa ndugu wa mwanamke aliyefunga ndoa na Ben aliyezungumza na gazeti hili kwa niaba ya ndugu wengine, wamechukizwa ile mbaya na kitendo cha Ben kulikalia kimya suala hilo huku kukiwa na mjadala kila kona. Alisema kibaya zaidi kwenye huo mjadala, ndugu yao amekuwa akitukanwa na kuambiwa maneno mengi ya shombo, lakini Ben amekuwa hataki kujitokeza na kueleza ukweli wa ndoa yao.

Ndugu huyo alifunguka kwamba, anaamini kuwa kama Ben angetaka ndugu yao asitukanwe kwenye mitandao ya kijamii kila kukicha, basi angejitokeza na kuanika ukweli kuhusiana na kile kinachosemwa juu ya ndugu yao.

Yaani mkeo kabisa anasimangwa kila kukicha kwenye mitandao ya kijamii halafu unanyamaza?  Kama kweli mtu una mapenzi ya dhati kwake, kwa nini ufichefiche? Kwa nini asiweke kila kitu wazi maana angeweka wazi, watu wangeheshimu uamuzi wake maana inavyoonekana ni kama anataka kujifanya siyo kweli bali ni filamu”.

Ndugu huyo alisisitiza kuwa ni kweli Ben amemuoa mchumba wake huyo wa siku nyingi.

Ndoa ilifungwa pale kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala (Boma) jijini Dar hivyo siyo kitu cha kusema kwamba ni filamu bali ni jambo linalotambulika kiserikali. Ukweli ni kwamba Ben alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na ndugu yetu kwa takriban miaka miwili sasa.

Cha msingi yeye atuambie kama hakumpenda ili tujue kabisa maana wanaume wa siku hizi ni shida sana. Inawezekana amemuona ndugu yetu yupo kwenye maisha mazuri, akatamani maisha zaidi kuliko mapenzi”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.