Ney wa Mitego Awashangaa Wasanii Wanaotumia Uchawi Kwenye Sanaa

Msanii wa Bongo fleva Ney wa Mitego ameibuka tena na kusema kuwa anashangaa sana pale anaposikia wanamuziki wanatumia ndumba kwenye kazi zao.

Katika mahojiano aliyoyafanya na Clouds FM kupitia kipindi cha XXL msanii huyo amefunguka yafuatayo kuhusiana na suala hili;

download latest music    

“Umefika muda Tanzania nzima inaamini katika kile ambacho ninafanya, hii ni ndele tosha ni zaidi ya ndele sijui mtu ambaye anaamini hivyo, halafu ndele huwa zina mwisho ukifika muda maana wewe ndo umemaliza hata uimbe vipi hata umshirikishe Yesu bado watu hawaelewi’.

Pia msanii huyo anayetamba na wimbo wake wa ‘Makuzi’ ameongeza kuwa msanii yoyote anayeamini kwenye uchawi huishia katikati ya safari na hupotea katika ramani ya muziki. Nay amekana vikali kujihusisha na ushirikina wa aina yoyote na kudai kuwa kwake kipaji alichojaaliwa na Mungu kinaongea chenyewe.

Wasanii wengi wa Tanzani wamekuwa wakijihusisha na imani hizo za kishirikina kwa hofu ya kupotea kisanaa ingawa wengi wao hukana hadharani lakini inasemekana wengi wao hutumia waganga wa kienyeji ili tu wakae kwenye sanaa hiyo kwa muda mrefu na kufnya kazi ambazo mashabiki watazipokea.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.