Nikki Wa Pili Afunguka Jinsi Alivyokutana na Mchumba Wake

Msanii wa hip hop nchini kutoka katika Kundi la Weusi Nickson Simon maarufu kama Nikki wa pili amefunguka na kuweka wazi Jinsi alivyokutana na Mpenzi Wake Joan ambaye Wiki iliyopita alimvisha pete ya uchumba.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Nikki aliweka wazi kuwa alikutana na mchumba’ke huyo kwenye kongamano la ujasiriamali lililofanyika katika Ukumbi wa Millenium Tower, Kijitonyama jijini Dar.

Wakati tunatoka kwenye kongamano ndipo nikamuona mtoto, nikamuomba namba huku nikijisemea mwenyewe huyu mtoto simuachi ni wa kumweka ndani kwa sababu alikuwa na vigezo vya mwanamke wa ndoto zangu”.

Nikki wa Pili amesema yeye na Mpenzi Wake wanatarajia kufunga ndoa mwakani mwaka 2019 Baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa miaka kadhaa ambapo Mpenzi Wake amemaliza elimu yake ya chuo kikuu  miezi michache iliyopita.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.