“Nilikuwa na akili ya kitoto” Muuza sura Masogange aeleza sababu ya kustaafu

Video vixen maarufu Tanzania – Masogange amefunguka kuhusu sababu ya yeye kuamua kuachana rasmi na mambo ya kuuza sura kwenye video za wasanii.

Mrembo huyo alieleza kuwa sababu kuu ya yeye kuuza sura kwenye video ilikua kupata umaarufu. Masogange alieleza kuwa kwa sasa amekomaa kiakili na hawezi uza sura kwani mpenzi wake pia hapendi akiwa video vixen.

download latest music    

“Wakati nauza sura kipindi kile nilikuwa na akili ya kitoto, yaani nilikuwa nataka na mimi niwe staa nijulikane. Nilikuwa nikiona wale dada zetu wanavyoonekana kwenye video na mimi nilikuwa natamani vile,lakini sasa hivi najuta kwasababu ustaa nao unanigharimu. Sio kwamba wasanii hawanioni hapana wananiona ila nimeamua kuachana na hiyo kazi, hata boifrendi wangu hapendi kabisa mambo ya kujulikana julikana,yaani mambo ya video queen hapendi kabisa. Nimekua mkubwa na mpenzi wangu hapendi,” Masogange alieleza.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere