“Nilikuwa na Ndoto Ya Kuwa Mwanasheria”-Gigy Money

Video vixen na msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu Kama Gigy Money ameibuka na kudai ndoto yake kubwa maishani ilikuwa kuwa mwanasheria.

Gigy Money ambaye alijizolea umaarufu kutokana na Umbo lake matata na vituko vyake kwenye mitandao ya kijamii lakini wimbo wake wa Nampa papa ulimtambulisha zaidi kwenye tasnia ya Bongo fleva.

download latest music    

Lakini hivi sasa Gigy Money anadai muziki haukuwa kwenye ndoto Zake Bali ameuvamia tu kutokana na maisha lakini yeye ndoto yake kuu ilikuwa kuwa mwanasheria.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari hivi karibuni Gigy Money amefunguka kuhusu ndoto hizo na kusema alikuwa anaipenda fani hiyo tangu akiwa mdogo kutokana na kuweza kumsimamia mtu kwenye ukweli bila kuyumbishwa.

Tangu mdogo nilikuwa napenda sana sheria sema sikusoma sana kwa sababu niliishia kidato cha pili lakini ndoto yangu kubwa ilikuwa kuja kuwasimamia watu kupata haki zao”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.