Nilimficha Mama Yangu Kuhusu Wimbo Wangu Mpya -Nay Wa Mitego

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Alisema’ Nay wa Mitego amefunguka na kuweka wazi kuwa alimficha mama yake kuhusu ngoma hiyo.

Wiki iliyopita Nay wa Mitego aliweka wazi kuwa mama yake mzazi ameshawahi kumtaka mwanaye aachane na muziki na kufanya biashara nyingine kutokana na kuhofia kitakachoweza kumpata kwa kuimba nyimbo zake za utata.

download latest music    

Katika Interview yake aliyofanya na Global Publishers, Nay ameweka wazi kuwa kutokana na kumuhofia mama yake Nay aliamua kumficha kuhusu kufanya ngoma hiyo.

Kiukweli nilifanya siri sikumueleza mama yangu kuhusu ule wimbo na mpaka natengeneza video yake sikumwambia lakini nilipokuwa studio nikawaza tu kwamba kuimba nyimbo za aina hii mama alishanikataza, huwa ananiambia niache kabisa kuimba kwa kuwa mimi nina watoto wananitegemea na familia kwa ujumla.

Kwa kuwa nimlificha aliisikia mtaani akanipigia simu na kuniambia niende nyumbani, nilienda pale na kumkuta akinisubiri kwa hamu sana ili kuniuulizia kwa nini nimerudia tena kuimba? Ikabidi nimueleweshe tu sikuwa na jinsi akanielewa,

Nilivyoutunga nikaishirikisha na menejimenti yangu nikaambiwa nimpe mwanasheria wangu aisikilize kwanza nikafanya hivyo alipoisikiliza akaniambia haina tatizo na vitu vichache tu nirekebishe nikafanya hivyo na hatimaye ikatoka”.

Nay wa Mitego ameshawahi kuingia matatizoni kwa aina yake ya uimbaji na ameshafungiwa nyimbo kadhaa na Basata.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.