Loading...

“Nimechoka Kusikia Kuhusu Prezzo” – Amber Lulu

February 13, 2018 at 07:38
“Nimechoka Kusikia Kuhusu Prezzo” - Amber Lulu

Video queen maarufu aliyegeukia fani ya muziki wa Bongo fleva, Amber Lulu amefunguka na kudai amechoka kuulizwa maswali kuhusu mpenzi wake ambaye ni raia wa Kenya supastaa anayejulikana kama Prezzo.

Amber Lulu na Prezzo walianika wazi kabisa mahusiano yao mwaka jana baada ya kukataa mara kadhaa kuwa hawana uhusiano hata mara baada ya kubambwa wakiwa wote hotelini.

Loading...

Tangu hapo wamekuwa wana uhusiano ingawa Amber Lulu anaishi Tanzania na Prezzo ni mkazi wa Kenya walidai wana uwezo wa kuwa na mahusiano mazuri tu bila wasiwasi wa kitu chochote.

Lakini mahusiano yao hayakuwa ya kimya kimya kwani mara kwa mara wameharibu hali ya hewa kwenye mitandao ya kijamii kwa kuweka picha ambazo mtu mwingine anaweza kukwambia hazina maadili kwani kuna siku walirusha picha ambazo ziliwaonyesha wakiwa watupu kabisa bafuni.

Pamoja na hayo yote kila mmoja amekuwa akisisitiza kuwa wanapendana na wana mapenzi ya kweli ambapo Prezzo ameshakiri kuwa wako ‘serious’ kiasi ya kwamba ameshaenda kumtambulisha Amber Lulu kwa mama yake mzazi na kusema mama yake amempenda kiasi ya kwamba wamekuwa marafiki.

Lakini jana wengi walishangazwa pale ambapo Amber Lulu aliwatolewa povu mashabiki zake kwenye mtandao wa Instagram baada ya kumuuliza kuhusu uhusiano wake na Prezzo kwa hivi sasa ambapo Amber Lulu aliandika:

Kila saa comments zenu mnamuongelea Prezzo tu nimechoka sitaki kusikia kuhusu mtu yoyote yule kila mtu ana maisha yake na pia kila kitu kinaenda kwa muda tu hebu tutafute hela sio kila saa kuongelea mb** tu # fu**”.

Baada ya povu hilo tetesi zilienea kuwa Amber Lulu na Prezzo wameachana ingawa hakuna kati yao aliyethibitisha hilo ila sababu iliyopelekea mpaka mashabiki kumuuliza sana Prezzo ni kwa sababu ameachana kabisa kumposti Prezzo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Share

Comments

  1. haha

  2. Prezzo awabadilisha kama chupi

  3. ana hasira mbona

  4. she seems heartbroken

  5. lo!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…

wavatar

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.