Nimekoma Kwenda Kujiuza India-Pretty Kind

Video vixen na msanii wa muziki wa Bongo movie Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind amefunguka na kudai ya kwamba hivi sasa hawezi kurudi tena nchini India kujiuza kama ilivyokuwa siku za nyuma bali anatulia kwa matumaini ya kuolewa.

Siku za nyuma Pretty Kind aliwahi kuweka wazi kuwa aliwahi kuishi nchini India ambapo kutokana na ugumu wa maisha alijikuta anafanya biashara za kujiuza mwili wake  ili kujiingizia kipato.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Pretty Kind alifunguka baada ya kuulizwa sababu ya utulivu wake wa hivi karibuni, huku wengi wakidhani amerejea kwenye biashara ya ukahaba nchini India ndipo aliposema kuwa kamwe hawezi kurudi nchini humo na maisha hayo ameshayasahau.

Unajua watu wakiona umetulia watakusaka kwa lolote, mimi ninakua sasa mambo yote nimeacha ninachotaka sasa ni mchumba wa kunioa hivyo nimejituliza ili nione kama nitafanikiwa kwa hili kwani maisha ya sasa huwezi kupata mume bila kutulia”.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.