Nimelipwa Milioni Saba Kufanya Shoo Bado Sijafulia- Wema Sepetu

Msanii wa filamu za Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kusema wazi kuw taarifa zinazosambaa kuwa amefulia hazina ukweli hata kidogo.

Wema Sepetu amekula shavu baada ya kualikwa kama mgeni rasmi kwenye Usiku wa Zanzibar Sweetheart utakaofanyika Zanzibar Beach Resort hivi karibuni.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Wema alisema tayari ameshalipwa kiasi cha shilingi milioni saba hivyo anamshukuru muandaaji wa tamasha hilo kwa kuona umuhimu wake na kwamba ametambua bado anapendwa.

Bado nina mashabiki wengi sana maana mpaka nimeweza kupata nafasi hii siyo mchezo, ninawashukuru sana waandaaji kunipa nafasi hiyo na hapo kila mmoja ataona muonekano wangu siku hiyo ya tarehe moja mwezi ujao”.

Kutokana na ukimya wake kwenye Mitandao ya kijamii imekuwa ikisemekana kuwa staa huyo amefulia na umaarufu Wake kuisha baada ya skendo yake iliyomchafua mwaka jana.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.