Nimeshawahi Kudate na Marco chali Lakini Kuna Wanaume Wengine Nawatamani-Sanchi

Mrembo Sanchoka ‘Sanchi World’ ambaye ni mwanamitindo na mfanyabiashara aliyepata umaarufu kwenye mitandao ya kijamii kutokana na urembo wake na shepu yake yakuvutia amefunguka na kutaja wanaume ambao angependa kuwa nao bongo.

Katika mahojiano aliyofanya na kipindi cha The Playlist cha Times FM Sanchi amefunguka kuwa anapenda mwanaume mwelewa, smple, mwenye upendo na pia awe na pesa za kutosha;

download latest music    

“Moja kati ya msanii wa Bongo anayenivutia ni John Makini ingawa sikuwahi kumwelezea hisia zangu lakini leo ndio atajua, lakini pia ninavutiwa na Ali kiba na Diamond na kwa nje ya nchi Nigeria ningefurahi kuwa na Davido”.

Pia Sanch alifunguka kuw hajawahi kuwa na uhusiano wa imapenzi na Idris Sultan kama watu wengi walivyodhani ila ameshawahi kuwa kimapenzi na mtu mmoja tu maarufu ambaye ni producer wa muziki Marco chali.

Sanchi pia alifunguka kuwa usumbufu mkubwa anaopata kutoka kwa wanaume mitandaoni ameshazoea kwa sasa kwani wa mara kwa mara. Lakini pia amesema havutiwi na wanaume wenye wivu na mwanaume ambaye hajiamini.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.