“Nina Maumivu Makali, Sitafuti Kiki” – Wastara

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma amefunguka tena na kuulilia uma wa Watanzania na kuwasihi wamsaidie kwa sababu yeye ni mgonjwa na yupo kwenye mauivu makali sana na kuwasihi kuwa hatafuti kiki kama watu wengi wanavyodai.

Wiki chache zilizopita Wastara aliomba msaada kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuwaomba watanzania wamsaidie kumchangia kiasi cha shilingi milioni 37 za Kitanzania ambazo zitatumika kwa ajili ya matiibabu ya miguu yake na mgongo ambao amedai umekuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.

download latest music    

Lakini baada ya kutangaza kuwa anahitaji msaada kumekuwa na muitikio tofauti kabisa kutoka kwa watu huku kila mmoja akiongea lake huku watu wengi wakisema kuwa Wastara amefanya vile ili kutafuta kiki kwa sababu anaweza kujihudumia mwenyewe.

Wastara amefunguka kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Friday Night Night Live cha East Africa TV na kusema kuwa anapata maumivu makali yanayotokana na kuumwa huku watu wakisema anatafuta kiki, anahitaji msaada wa Watanzania:

Yaani hapa mtu anaweza akaniumiza kwa maneno anaweza akaniumiza kwa vitendo Kwa sababu yeye anaamini kwa kichwa chake na mawazo yake kwamba yule mtu anaamini kuwa mimi nimelala kitandani siumwi au nimepotea kwenye sanaa natafuta kiki, kiki ya kujifunua nguo nikapiga picha mguu wangu ambao umekatika kwenye gazeti? Jamani hii sio kiki nipo kwenye maumivu makali na ninahitaji msaada wenu lakini pia siwezi kulazimisha mtu kuamini au hata wasanii wenzangu kuamini kuwa naumwa”.

Wastara alianza kusumbuliwa na matatizo ya mguu miaka michache iliyopita baada ya kupata ajali ya gari ambayo ilimpelekea kukatwa mguu mmoja lakini miaka ya hivi karibuni alianza kusumbuliwa na mguu mwingine ambapo pia amekuwa akipatwa na maumivu ya mgongo.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.