Nipo Tayari Kuzaa Watoto Wanne na Iyobo-Aunty Ezekiel

Muigizaji wa Bongo movie na Mfanyabiashara Aunty Ezekiel amefunguka na kuweka wazi mahusiano yake na Mpenzi Wake ambaye ni dansa wa WCB Mose Iyobo.

Aunty na Iyobo wamefanikiwa kuzaa Mtoto mmoja wa kike anayeitwa Cookie ambapo kwenye mahojiano yake na Global Publishers, Aunty ameweka wazi sababu za kumpa binti yake jina la Cookie.

download latest music    

Unajua maana ya Cookie ni vibiskuti vile vidogo, lakini vitamu sana, sasa nilipomzaa tu niliona nimepata kitu kitamu sana kuliko chochote hapa duniani, nikaamua tu kumpa mtoto wangu jina hilo kumuonesha kwamba yeye kuwa mwanangu ni utamu tosha kwangu”.

Lakini pia Aunty Ezekiel alisema Kama walivyokuwa wazazi wengi ana mipango mingi juu ya binti yake huyo hasa inapokuja Suala la elimu yake:

Nimepanga aje kuwa msomi huko mbeleni na ndiyo maana nimetenga pesa zake nyingi tu za kumsomesha sasa hivi mpaka darasa la saba bila bugudha yoyote alafu nyingine ya kuendelea na masomo ndiyo nimeanza kuweka sasa“.

Alipoulizwa kuhusu kuongeza mtoto mwingine na baba watoto wake huyo Aunty aliweka wazi kuwa yupo tayari kuwa na watoto wengine watatu lakini endapo tu muda maalumu utafika:

Natamani sana, lakini bado kidogo, kuna vitu navikamilisha alafu ndiyo nifikirie kuzaa mtoto mwingine, siyo mmoja hata watatu kwa sababu mimi napenda sana watoto”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.