Nisha Amponda Bwana wa Snura Adai ni Kiben-10 Kula Kulala

Muigizaji  wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu mtandaoni Nisha Bebe amewatolea povu wanaume wote wanaopenda kulelewa na wamama watu wazima ambao wanajulikana kama viben-10 au Marioo au Serengeti boys.

Wiki chache zilizopita kuna stori ilitrend mtandaoni kuwa Nisha kaporwa kiben-10 chake na msanii wa Bongo fleva Snura Majanga. Kijana huyo anayejulikana kama Minu Calypto alikuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Nisha kwa mara ya kwanza ambaye alikuwa na umri mdogo kuliko yeye.

download latest music    

Minu hivi sasa kajiweka kwa mwanamke ambaye ni wazi kuwa ni mkubwa kuliko yeye maana Snura anaonekana kama mtu mzima kwa Minu. Baada ya picha za Minu na Snura kusambaa siku ya Valentine’s Day na kuthibitisha uhusiano wao, Nisha amewatolea povu zito viben-10

Kupitia kipindi cha FNL ya East Africa Tv, Nisha amemtolea povu aliyekuwa bwana ale Minu na kumuita kula kulala ambapo aliwaandikia:

Mnazingua kwaiyo mnadhani mimi naweza kutiwa stress na mwanaume kula kulala?nimeanza kusafiri tangu 2013 now ni 2018, Niacheni jamani tafadhali”.

Nisha amesema hawezi kukaa na kuumia kisa mwanaume ambaye alikuwa hamsaidii kitu chochote maishani mwake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.