Nisha Atolewa Povu na Mke wa Mzungu

Msanii wa Bongo movie aliyegeukia tasnia ya Bongo fleva Salma Jabu maarufu kama Nisha ametokewa povu zito na mke wa mzungu Anatoly Shmakov aliye trend naye Kwenye social media wiki iliyopita.

Mwanamke huyo amejitambulisha kwa jina la Felista ambaye amedai ni mke wa mzungu ambaye alionekana Kwenye mitandao ya kijamii wiki iliyopita akiwa na Nisha ambapo Nisha alidai ni mpenzi wake.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers Felista amedai ameshangaa kumuona Nisha anamuita mzungu yule mpenzi wake wakati yeye ni mume wake halali wa ndoa kabisa:

Kwanza mimi sikuona picha hizo mwanzo, ila nilipigiwa simu na rafiki yangu yupo Zanzibar na kuniuliza kama nimeziona hizo picha mtandaoni.

Kwa kweli nilishtuka sana baada ya kuziona picha hizo kama mke na yule ni mume wangu imeleta shida sana kwenye familia.

Nilijaribu kumuuliza mume wangu kuhusiana na picha hizo na yeye ilimshangaza kwani alipokuja Nisha nyumbani kwangu, alimuomba awe kwenye video ya wimbo wake na zile picha zipo kwenye video ya huo wimbo lakini haikuwa makubaliano ya kutangaza vile mitandaoni kuwa ni mwanaume wake. Sijapenda kwa kweli alivyofanya”.

Lakini mwanamke huyo ameweka wazi kuwa yeye na mume wake sasahivi wako vizuri:

Sasa hivi tupo sawa tumeyamaliza kifamilia maana ilikuwa ni tatizo sana“.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.