Nisha- Biashara Zimenipa Mafanikio Kuliko Filamu

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Salma Jabu maarufu kama Nisha amedai biashara zake za nguo zimeweza kumpatia mafanikio ya haraka ambapo mpaka sasa tayari ameshanunua nyumba na magari ya kutembelea.

Nisha amefunguka Kwenye mahojiano na Bongo 5 na kuweka wazi kuwa alipokuwa anafanya Bongo Movie alikuwa anapata pesa ndogo ndogo sana ambazo aliziweka na kuanzisha biashara yake kuuza nguo ambayo amekiri kuwa imempa mafanikio mengi sana.

download latest music    

Mimi filamu nimeanza kucheza kama hausegirl nikilipwa sana labda elfu ishirini lakini pesa hiyo hiyo ndio imenipa leo hii biashara yangu ya nguo ambayo inanifanya mimi kila siku niende benki kwenda kuweka pesa”.

Lakini pia Nisha ameanika mali zake alizozipata Kupitia biashara zake.:

Kwa kweli mimi nina nyumba nina magari kama unavyoona nimepaki jingine pale nje kwaiyo namshukuru Mungu biashara zangu ndio zimenipa mafanikio sana”.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.