Nisha: Mnaosema Sina Shepu Nimepigwa Pasi Mnikome

Muigizaji wa Bongo movie Nisha amibuka tena na kumwaga povu zito kwa mashabiki zake baada ya kudai ameona maoni ya watu wengi wakimwambia kuwa kapigwa pasi yaani hana makalio.

Nisha alitoa povu hilo siku za nyuma kidogo ambapo ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa ambapo aliweka picha zake ambazo alikuwa amevaa gauni lake refu mpaka chini lililochora mwili wake ipasavyo ndipo kila mtu alipoanza kumsema hana mwili mzuri wa kuvalia gauni lile kwani amepigwa pasi.

download latest music    

Nisha alitokwa na povu zito baada ya kuona watu wanamsema na kudai hana shepu hivyo aliibuka na kusema shepu yake anaipenda ilivyo vile vile kwani sio feki kama shepu za wanawake wengi hapa mjini amabapo wengi wao hutumia madawa ya mchina kuongeza makalio:

Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika ujumbe huu:

Halafu nyie mnaosema sina shepu sijui nimepigwa pasi mnikome, tukivaa vigodoro maneno mtu akivaa kama alivyo maneno, hemu chunguzeni wanawake wote wazuri duniani na wenye mashepu na status zao ndio wale wanaoishia kupiga picha za uchu, kujiuza, kuishi kwa kutegemea mabwana then angalia status za waliofanikiwa wote. Omba Mungu akupe afya njema, akili, imani, heshima, upendo, maarifa na kipato Sote tumeumbwa kwa mfano wake. Kutengeneza shepu ni dola 6000 tu lakini napenda Mungu alichonijalia na pia najivunia na nijajikubali”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.