Nisha- Wasanii Wanapenda Kiki Sababu Watanzania Wanasapoti Kiki Kuliko Kazi Zao

Muigizaji wa Bongo movie aliyegeukia sanaa ya Bongo fleva Salma Jabu maarufu kama Nisha ameibuka na kuwatetea wasanii wanaofanya kiki sana na kudai Watanzania wanapenda sana kiki.

Wiki iliyopita Nisha alishika headlines sana baada ya kusambaza picha Kwenye mitandao ya kijamii akiwa na mzungu ambaye alidai ni mume wake ambaye baadae ilikuja kujulikana kuwa ni mtu aliyefanya naye video tu.

download latest music    

Baada ya mashabiki kumjia juu na kumtuhumu kwa kupenda kiki Nisha amewatolea povu na kudai yeye pamoja na wasanii  wengi wanapenda kiki kwa sababu mashabiki wanafuatilia umbea unaowahusu kuliko kazi zao.

Nisha alimwaga povu hilo Kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuandika:

Watanzania wengi wanawasema wasanii wengi kuhusu kiki, Ila wanasahau kuwa wao ndio namba moja wanapenda umbea kuliko kazi zetu.

Tazama tukitoa umbea tunavyosapotiwa kuliko kazi, Yeye ni wimbo ulionifunza mengi”.

Mara ya mwisho Nisha alitoa wimbo wake wa kwanza ambao ulisindkizwa na kiki ya kuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na Ex wa Wolper Brown.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.