Njia Sahihi Ya Asili Ya Kukuza Nywele Zako

1.Zifahamu aina ya  nywele zako

kitu cha kwanza kujua ni kizifahamu nywele zako, kuna watu wanakaa na nywele bila kujua nwele zake ni za iana gani,Jinsi ya kujua aina ya nywele zako , chomoa nywele moja katika kichwa chako na uhakikishe imetoka na kale kamzizi kanakokuwa na rangi ya weupe ivi, kisha dumbukiza unywele huo kwenye glasi yenye maji na angalia kama unywele uo unaleta matokeo gani,kama itazama mara moja na haitanyanyuka tena basi jua nywele yako inanyonya unyevu kwa haraka ivyo inaitaji kuwa na unyevu unyevu na kama .

download latest music    

2.Linda umyevu wa nywele zako.

kama ilivyo kiu kwa binadamu, ndivyo hivyo nywele huitaji maji, kwaio kipindi unapokuwa unaosha nywele zako kabla ya kuzipaka mafuta ya kulinda nywele zako jitahidi kuwa una fanya  deep condition ili kuzifanya zibaki na unyevu .

3.Usafi wa ngozi na nywele zenyewe pia.

Kuna watu wanasema kuwa nywele zikioshwa mara kwa mara zinadumaa, lakini ulishawahi kujiuza endapo wewe utakaa bila kuoga.Nywele zinahitajika kuwa safi na ngozi yake pia ili kuifanya ngozi kufunguka na sio kufungwana ule uchafu wa mafuta.Matundu yanapokuwa wazi ndio ufanya nywele kuweza kujitokeza ivyo jitahidi kuosha nwele na kuhakikisha kuwa ngozi yako ni safi.

4. Chagua Mafuta  bora ya kupaka

Jitahidi kuchagua mafuta mazuri kwa ajili ya nywele zako.sio kila mafuta yanafaa kupaka katika nywele zako ingawa mafuta ya nazi ni mazuri zaidi au mafuta ya olive.kitu kizuri ni kuzijua nywele zako kwanza ndipo utaweza kujua pia bidhaa bora ya mafuta kwa ajili ya nywele.Ukishindwa ni bora kuonana na wataalamu wa mambo ya urembo.

5.Epuka kuzisumbua nywele kila wakati.

Ni vizuri kuwa unachana nywele kwa muoekano mzuri wa sura yako na nwele pia, lakini kitendo icho ufanya nywele kuwa zinapuputika sana,jitahidi kuwa unazisuka ili kuzifanya zikue pia.Kuchana chana nywel ni kuzisumbua.

Inawezekana inakuwa ni ngumu kutambua nywele zake zinahitaji mafuta ya aina gani, au bidhaa gani ni bora zaidi kwa nywele zako, ni vizuri pia kuonana na wataalamu ili kuzisaidia nywele zako.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.