Norah Atangaza Kuachana na Uigizaji

Msanii mkongwe wa filamu nchini Nuru Nasorro maarufu kama Norah Nassoro ametangaza kuachana na kuigiza filamu.

Nora ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram huku akiwakosoa baadhi ya wasanii wa sasa wa filamu kuwa wamejawa na utandawazi, jambo ambalo linawapelekea kufanya mambo yasiyokuwa na maadili kwenye mitandao ili kusudi wapate kusifiwa, kujulikana na kupendwa.

download latest music    

 

Nimeacha historia kwenye maisha yenu, kila mnapo nikumbuka kumbukumbu nzuri za furaha zinawajia kwenye vichwa vyenu, mpaka mnatamani enzi hizo zingekua zinarudi. Namshukuru MUNGU wangu sana kwa hili kwani ni kitu kizuri ukifanya kitu na watu wakakukumbuka kwa mazuri kiukweli ninapata furaha mnoo, ambayo haielezeki…

Japo najikuta najisikia vibaya wengine wanaposema walikua wanafukuzwa kwenye ‘sitting room’ za watu lakini ilibidi wakae madirishani na ikibidi wakate madirisha ya watu, wengine walikua wanakalishwa chini au inawabidi wafanye kazi ili jioni inapofika waangalie kipindi. Ninawatangazia rasmi nimeacha kuigiza”.

Lakini pia Norah ametoa shukrani zake za dhati kwa mashabiki zake :

Mapenzi yenu yalikuwa sio ya kawaida wallah, hata nikifa leo kazi ilio nileta duniani ya kuwa burudisha na kuwafundisha nilifanya kwa ufasaha. Ama kweli enzi haziwezi kurudi, sasa hivi dunia imekua ya utandawazi watu wamekuwa wakilazimisha kupendwa, kusifiwa, kujulikana, inafikia wakati maadili hamna, mazoea ya kukaa pamoja kama familia na kuburudika na kujifunza”.

Nimeacha alama ambayo haitofutika daima niko hai au nimekufa, alama ambayo hata kwa Mungu ninacho cha kujitetea na akanielewa kwa kuwa siku lazimisha umaarufu ulikuja wenyewe, sikudanganyika na dunia bali niliishi kadri umri ulivyo nihitaji. Mara zote niliipigania heshima yangu kwenye kila kitu kama binadamu nilikosea lakini sio kwa makusudi eti ili niitawale dunia”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.