Nuh Mziwanda: Siwezi Kurudiana na Shilole

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nuh Mziwanda amefunguka na kudai Kuwa habari zilizosambaa kuwa amerudiana na Shilole sio za kweli kwani hawezi tena kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake hspo mwanzo.

Shilole na Nuh waliachana kipindi cha hapo nyuma ambapo baada ya kuachana waliingia katika vita ya kurushiana maneno mtandaoni ambapo Nuh alidai kuwa wakati wapenzi Shilole alikuwa anamnyanyasa kwa sababu yeye ndio aliyekuwa anatengeneza pesa kati yao lakini pia Shilole alimtuhumu kuwa Huh alikuwa ana michepuko ndio sababu ya yeye kumpiga.

download latest music    

Baada ya kuachana kila mmoja aliendelea na maisha yake binafsi huku Shilole akianzisha mahusiano na kijana anayeitwa Uchebe na Nuh Mziwanda alifunga ndoa na mrembo anayekwenda kwa jina la Nawal lakini baadae walikuja kuachana na Nawal kuolewa na mwanaume mwingine.

Kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv, Nuh Mziwanda amekana tetesi za yeye kurudiana na Shilole na kudai kuwa hawezi kurudiana na Shilole tena bali anawatakia maisha mema yeye na mumewe Uchebe kwani penzi lao ni zilipendwa lakini pia amedai kuwa zile picha zilizosambazwa mtandaoni wakiwa wamelala kimahaba zilikuwa ni picha ya siku nyingi sana wakiwa wapenzi na sio yeye aliyezisambaza kama Shilole alivyomtuhumu kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya Jana.

Lakini Nuh pia alifunguka na kudai kuwa tetesi za Kuwa amerudiana na mama wa mtoto wake, Nawal sio za kweli bali wanapatana kwa sasa kwa ajili ya kumlea binti yao na sio mambo mengine ya kimapenzi amedai kwa sasa hana mpenzi yoyote.

 

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.