Nyota Ndogo Aguswa na Ugonjwa wa Hawa.

Mwanamuziki kutoka kenya anayejulikana kwa jina la Nyota Ndogo aliyewahi kutamba kwa wimbo Kuna watu na viatu ameamua kuwapa makavu wasanii wa bongo na kuwataka washirikiane kumsaidia msanii mwenzao Hawa wa ntarejea ambaye anasumbuliwa na tatizo la Ini.  Nyota ndogo ambaye ameonekana kuguswa sana na tatizo lililomkuta Hawa ameamua kuandika waraka mrefu akiwataka watanzania hususani wasanii kushirikiana ili aweze kutibiwa.Kupitia akaunti yake ya instagramu aliandika Hivi:

Najua nitasutwa lakini ni sawa tu. Sijui sanaa ya nanzania mumempangia nini huyu mrembo kuhusu ugonjwa wake.kitu kikiekwa kwenye mtandao ni kitu cha dunia nzima.watanzani nimekua niwakubali kwa umoja wenu mnavyoshirikiana basi shirikianeni kwa huyu pia ni wanu.hivi ndio tunafanya mwenzetu msanii akiumwa na tukijua bila hata kuishirikisha serekali kuna kuna watu wawili kwenye sanaa wanawapigia wasanii siku kuwaambia tuandaeni show kubwa hela zimsaidie mgonjwa kwenye matibabu ama msiba kama unaitajika.na hivyo inakua rahisi kusaidiwa. Mbona radio nyingi tu tz mbona wasiandae show na radio zikubali kutangaza hii show jamani mtoto atibiwe,AMA NDIO ILE MSEMO WA NAENDA KWA NINAE MJUA?.hapana sio hivyo saidiane wasanii kwakweli.mimi pia kama msanii naweza kua Sina hela nyingi but nikiweza kuasiliana na hii famili nitatuma uwezo wangu jamani kidogo nilichonacho nitatuma.ENDAPO NIMEMKOSEA YEYOTE KWAKUANDIKA HII NAOMBA SAMAHANI..

download latest music    

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.