Ommy Dimpoz Adaiwa Kumpa Maneno Makali Baba Yake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amedaiwa kumchimba mkwara mzito baba yake mzazi Faraji Nyembo.

Gazeti la Ijumaa linaripoti kuwa Ommy Dimpoz alimtumia ujumbe baba yake huyo na kumpiga mkwara mzito kuwa kuanzia sasa asizungumzie kuhusu afya yake au mambo yoyote yanayomuhusu.

download latest music    

Siku za nyuma kidogo kuna taarifa zilisambaa kuwa Ommy Dimpoz alizidiwa na kurudishwa tena nchini Ujerumani kwa ajili ya matibabu taarifa ambazo baba yake na Ommy alithibitisha.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Baba Dimpoz alifunguka kuwa ni kweli amepata ujumbe huo mzito ambao umemuhuzunisha kwani hakutarajia ingekuwa hivyo.

Dimpoz amemtumia mtu ujumbe aniletee mimi kwamba kuanzia sasa siruhusiwi kuzungumza chochote kuhusiana na yeye hivyo nimenawa mikono kwa kweli sasa.

Nilikuwa namzungumzia kwa uzuri tu mwanangu na kumtetea kwa wale wanaomsema vibaya lakini kaona nilikuwa nafanya vibaya, nimekubaliana naye kwa kuwa hata hainisaidii kitu chochote katika maisha yangu”.

Inasemekana kuwa Dimpoz hataki watu wajue kuhusu afya yake vile anavyoumwa kwa hiyo anaona baba yake kama anamuharibia wakati alitaka kuufanya ugonjwa huo kuwa siri, ndiyo maana amepata hasira.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.