Loading...

Pajamas, Trending Fashion Kwa Kina Dada

October 16, 2017 at 13:40
Pajamas, Trending Fashion Kwa Kina Dada

Kuna fashion imekuwa ikitrend kwa muda kidogo , wadada wa mjini wamekuwa wa kivaa pamajas na kutoka katika matukio tofauti, ingawa hivi juzi pia nguo hii iliwaacha baadhi ya watu midomo wazi baada ya kuvaliwa na Zari The Bossy.

Loading...

Zari alivaa nguo hii na kuwa na muonekano huu katika uzinduzi wa duka jipya la Mlimani City mali ya Gsm.Lakini watu katika mitandao walimkosoa na kuona kama amevaa nguo ya kulalia katika event kubwa kama ile.

Nguo hii ni moja ya fashion iliyo-trend sana katika mitandao kwa wakina dada, wengine wakivaa na raba chini au kiatu kirefu.Hawa ni baadhi ya mastaa wakubwa waliovaa kabla ya Zari lakini haikuwa imeongelewa kama ilivyoongelewa baada ya kuvaa Zari.

Millen Magesse alivaa nguo hii kipindi cha ujauzito wake , ni zaidi ya miezi mitaano imepita.Chini alipiga na raba zilizomfanya haonekane maridadi zaidi.

Vera Sidika alishawahi kuvaa aina hii ya nguo,huku akichagua rangi inayoenda na mwili wake na alioneka kuwa perfect!!

Vannesa Mdee akiwa ndani ya kivazi hiki cha  pajamas ikiwa ni trend fashion na alitoka vizuri  kwenye event kubwa ya utoaji wa tuzo za  billiboard music awards,chini akiwa amevaa high heels.

Kris Jenner, mama mzazi wa mwanamitindo maarufu Kim Kardashian, ni mmoja wa watu maarufu duniani ambae alishawahi kuonekana akiwa ametoka na style ya pamaja.

Tahiya, mmoja wa video queen wanaofanya vizuri bongo, alishawahi kutoka na kivazi hiki cha pamaja pia.

watu wengine maarufu kama jokate,k-lyn,rihana walishawahi kuonekana na kivazi cha pjama katika events kubwa , kwaio ni fashion inayoweza kumfit mwanadada yoyote ilimradi uweze kupangilia jinsi ya uvaaji wako na rangi gani inayoweza kukufaa ili uweze kuwa na muonekano mzuri.zipo za maua, zipo za mistari lakini pia zipo za rangi moja.

 

 

Share

Comments

  1. Si walisema ya kulala hayo magauni

  2. Kila mtu ataanza kuyavaa maana zari kavaa

  3. Mazuri sana

  4. Hii ndio habari kuu mjini

  5. Ziko poa sana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Fashion

Loading…

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.