Patcho Mwamba Amuhurumia Lulu Na Maisha Ya Jela

Ingawa muda kidogo umepita tangu msanii wa bongo movies Elizabeth Lulu Michael kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya  kuua bila kukusudia kutokana na kifo kilichotokea miaka mitano iliyopita kikimuhusisha Lulu Michael kumuua msanii mwenzie Steven Kanumba ambae alikuwa nae katika mahusiano ya kimapenzi na kutokea ugomvi na kusabaisha kifo hicho.

Moja ya watu waliokuwa karibu sana na marehemu kutokana  na kufanya kazi nyingi pmaoja Patcho Mwamba amefunguka na kusema kuwa amekuwa akimuonea huruma sana Lulu kutokan na maisha ya jela jinsi yalivyo ukizingatia Lulu bado ni mdogo na miaka miwili kwake ni mingi inagwa pia anapaswa kushukuru kwa sababu kesi za aina hiyo hukumu yake huwa ni kubwa zaidi ya ile aliyopewa yeye.

download latest music    

Msanii huyo wa bendi ya Fm Academia amesema kuwa katika sehemu zote, jela sio sehemu nzuri kabisa  tena miaka miwili sio michache.

kwakweli jela wala sio kuzuri na mimi ninamuonea lulu huruma sana, lakini niseme tu lulu pia anapswa ashukuru mungu kwa namna  namna mabvyo hukumu zingine za aina hiyo zinakuwa sio kama yake , hukumu aliyopewa ni ndogo, tumeshuhudia watu wengi wamefungwa miaka mingi zaidi yake.-Aliongea Patcho Mwamba.

Tarehe 13 November , Lulu alipokea hukumu yake na kuanza kufungo mara moja baada ya hukumu hiyo kutolewa huku ikisemekana kuwa mwanadada huyo amekataza familia yake na mwanasheria wake kufanya mchakato wowote wa kukata rufaa kwa sababu anaona ni bora kutumikia kifungio hicho na kisha kuwa huru zaidi kuliko kukumbana na maneno ya watu.

Baadhi ya watu wa karibu wa marehemu Kanumba ikiwepo wazazi wake, walilalamikia hukumu hiyo na kusema kuwa hukumu hiyo kwa Lulu na kwa mtu aliyeua  haikuwa swa kwa sababu wanaona kuwa  ni ndogo sana.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.