Penzi la Linah na Baba Watoto Wake Ladaiwa Kuvunjika

Penzi la staa wa Bongo fleva Linah Sanga na mwanaume aliyezaa naye mtoto mmoja anayejulikana kama Mchomvu linadaiwa kuvunjika pamoja na kuwa katika tarartibu za ndoa.

Global Publishers wanaripoti kuwa Penzi la wawili hao limeota  mbawa wakati wakiwa kwenye taratibu za kufunga ndoa.

download latest music    

Linah na mzazi mwenzake walianza kuingia kwenye mgogoro baada ya mwanadada huyo kujifungua mtoto wake huyo. Ilisemekana kwamba, mara kadhaa wamekuwa wakikalishwa chini na kuyamaliza mambo yao kichinichini bila mtu yeyote kujua kisha wanaendelea na uhusiano kama kawaida.

lakini inadaiwa kuwa ugomvi wa wawili hao mara nyingi ulikuwa ni wivu wa kimapenzi hivyo hicho ndicho kilichosababisha uchumba wao huo kuvunjika ambapo mpaka sasa kila mmoja anamuona mwenzake mchungu.

Hakuna cha zaidi kilichovunja uchumba ni wivu tu ndiyo ulikuwa ukiwatafuna wote wawili mpaka kufikia hatua ya kuvunjika kwa penzi lao”.

Baada ya taarifa hizo gazeti hilo lilimsaka Linah na kumuhoji kuhusu taarifa hizo ambapo alifunguka na kukiri kuwa hayupo na mpenzi wake:

Hivi kwani ukizaa na mtu mpaka muoane? Ndio hivyo Lakini Sitaki kuongea zaidi kuhusu iyo ishu”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.