Loading...

Peter Msechu Afunguka Jinsi Alivyonusurika Kifo

July 23, 2018 at 08:42
Peter Msechu Afunguka Jinsi Alivyonusurika Kifo

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Peter Msechu amefunguka na kuweka wazi jinsi alivyo nusurika kufa kutokana na uzito mkubwa uliokuwa umemuelemea.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, baada ya kuulizwa juu ya kupotea kwake kwenye gemu kwa kupunguza vurugu za kuachia kazi kama ilivyokuwa mwanzo, Msechu alisema yupo ‘busy’ anahudumia kwanza afya yake.

Loading...

Ni kweli nipo kimya kwa maana kwenye gemu kwa sasa ninanusa nusa tu tofauti na ilivyokuwa zamani. Nafanya hivi kwa sababu sasa ninahudumia afya yangu.

Unajua nilikuwa nimejiachia sana kiasi kwamba nikawa nimefikisha uzito wa kilo 184 jambo ambalo lilikuwa ni hatari sana kwangu”.

Msechu alidai baada ya kufikisha uzito huo mkubwa alijikuta katika wakati mgumu kwani kuna kazi ambazo alikuwa hawezi kuzifanya tena:

Niliamua kwenda hospitali kwa ajili ya kufanya vipimo. Baada ya kufanyiwa uchunguzi niliambiwa tatizo ni uzito maana nina kilo nyingi pamoja na mafuta ambayo ilikuwa imefika hatua yamezunguka moyo.

Nikaambiwa kwa hali ilivyokuwa inakwenda, muda wowote ningezimika tu ghafla kama nisipochukua jitihada za dhati za kupunguza mafuta”.

Msechu amedai tangu hapo kutokana na maelekezo ya daktari ameweza kukata jumla ya kilo zaidi ya ishirini.

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…