Petit Alikataa Kuwa Muoaji Kwenye video Yangu :-Karen

Mwanadada karen amefunguka na kupangua tetesi za kutembea na Petit man kama ambavyo katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakisema na pia mke wa awali wa Petit kusema kuwa anavyojua yeye ni kuwa mwanadada karenamekuwa akiishi kinyumba na Petit kwa muda sasa.

Karen anasema kuwa yeye na petit walikuwa marafiki na wataendelea kuwa marafiki na hata katika video ya washa Petit alikataa kata kta akuwa bwana harusi  na kwamba ilichukua muda mrefu sana mpaka kumfanya akubali swala hilo.

download latest music    

Akielezea kwa kirefu zaidi, Karen anasema kuwa walipokuwa wakirekodi weimbo huo studio Petit alikuwepo kwa shughuli zake na alipousikia wimbo alisema kwa utani kuwa huo wimbo inabidi kuwe na bwana harusi na kusema kuwa yeye atakuwa lakini kumbe hakuwa serious na swala hilo.

Hivyo basi hata baada ya maandalizi ya shooting kuisha walijikutwa wakimtegemea petit kama bwana harusi kitu ambacho kiliwafanya kumtafuta na alikataa akasema kuwa alikuwa akitania wala hawezi kufanya hivyo.

Karen anasema kuwa ilichukua muda na nguvu kumshawishi akubali na hata alipokubali  hakutaka kutangaza kwa kila mtu kuhusu ilo na hata picha zilivyovuja alitumia nguvu kuelezea watu wake wa karibu na ndugu zake pia.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.