Petit Man Ayatetea Mapishi Ya Mke Wake Esma

Hamad Manungwa maarufu kama Petit Man ameibuka na kumkingia kifua mke wake Asmah Khan ‘Esma Platnumz’ baada ya kutuhumiwa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa hajui kupika.

Siku chache zilizopita Esma aliposti picha ya chakula alichomuandalia mume wake kama futari lakini mambo yaligeuka kwani mashabiki walimjia juu na kumsema hajui kupika.

download latest music    

Lakini Petit ameibuka na kusema wote wanaotokwa na maneno kuwa mke wake hajui kupika hawajui wanachokiongea kwani yeye ndio anajua anapikiwa nini kila siku.

Petit alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers ambapo alizidi kufunguka:

Unajua mimi sibishani hata siku moja na watu wa mitandaoni kwa sababu najua wazi sio mke wangu aliyepika ile futari. Akipika yeye chakula kinakuwa cha uhakika, nikila nasikia raha hadi najivunia kumuoa, hao wanaosema Esma hajui kupika, wana lao jambo”.

Baada ya Tuhuma hizo kuzidi Esma aliposti chakula kingine huku akisisitiza kuwa chakula watu walichokiona hakupika yeye.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.