Picha za Hamisa na Diamond zavuja

Ni zaidi ya mwaka sasa  upite tangu kuwepo na tetesi za kuwepo kwa mahusiano kati ya msanii wa Bongo Fleva Diamond Platinumz na video queen maarufu wa Bongo Hamisa Mobeto.Hamisa ambae amekuwa akitishia uhusiano wa kimapenzi kati ya Diamond na mzazi mwenzie  na msanii  huyo Zari The Bosylady,hata hivyo  miezi michache iliyopita  Hamisa alijifungua mtoto wa kiume aliempa jina la Prince Adbul Nasib  au’ Tanzania baby’, mtoto ambae inasemekana  kuwa ni mtoto wa Diamond Platinumz huku akiongeza idadi ya watoto wa msanii huyo mkubwa kuwa watatu .Tangu kuwepo kwa tetesi hizo Diamond mwenyewe amekuwa akikanusha tetesi hizo na kusema  kuwa hana uhusiano wowote na video queen huyo ,zaidi ya mahusiano ya kikazi tena hasa walipokutana katika kushoot video ya wimbo wa ‘salome’ , wimbo  ambao uliozua mambo mengi na ndipo tetesi za wawili hao kutoka ulipoanza kusambaa.

Zari , mama mzazi wa watoto wawili aliozaa na Diamond amekuwa akijikuta katika vita ya kimtandao na mashabiki na hata Hamisa mwenyewe huku  sababu kubwa ikiwa ni kuwepo kwa   tetesi hizo. Pamoja na hayo yote nata   Hamisa mwenyewe  amekuwa akirusha madongo  hewani bila kudhibitisha  moja kwa moja ukweli wa tetesi hizo.

download latest music    

Wapo mashabiki wanaosema kuwa wawili hao (Hamisa na Diamond ) wamekuwa wakionekana pamoja baadhi ya maeneo, lakini  pia ukiachana na hayo, kipindi ambacho Hamisa Mobeto amejifungua wanafamilia wa Diamond walikuwa ni moja ya watu wa karibu walikwenda kumtembelea Hamisa  hospitali ambapo alilazwa mrembo huyo.

Baada ya tetesi hizo kuwepo kwa muda sasa, zimevuja picha  zinazosadikika kuwa ni picha za Diamond na Hamisa Mobeto wakiwa chumbani , huku mkono wa diamond wenye kuonyesha tatoo yake, hata hivyo picha zingine zinazoendelea kusambaa ni zile zinazimuonyesha Hamisa yupo kwenye chumba ambacho ni chumba cha kulala cha Diamond na mama watoto wake huku eneo ilo likionekana kufafanana kabisa na lile ambalo Zari amekuwa akipost picha katika ukurasa wake wa instagram kama sehemu yake ya kulala pia.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.