Pretty Kindy Alalamika Maisha Magumu

Baada ya kupita kama wiki mbili tangu kufungiwa kwa kazi zake za kisanii kwa upande wa muziki na filamu, msanii w amuziki nchini susani michael marufu kama Pretty Kindy amefunguka na kulalamika kuwa kwa sasa maisha yamekuwa magumu sanakwa upande wake kutokana na kusimama kwa kazi zake ambazo ndizo alizokuwa akitegema zimuingizie pesa kwa muda wote wa maisha yake ya sanaa.

Pretty kindy anasema kuwa ingawa muda bado sana lakini anaona jinsi gani kufungiwa kwa kazi zake kunavyomfanya akae na maisha magumu sana kwa kipindi chote ambacho atakuwa hana kazi ya kufanya zaidi ya kutegema ndugu ambayo ni kazi ngumu zaidi.

download latest music    

Pretty kindy anasema kuwa kwa sasa amekuwa omba omba kwa ndugu na marafiki zake kitu ambacho anahisi itafika sehemu watamchoka kwa sababu kazi ya sann ndio ilikuwa ikimuingizia kipato katika maisha yake.

Kwa kweli nimenyooka ingawa ni kwa siku chache tu nimekaa na zilizobaki ni nyingi mno lakini naona kabisa nimenyooka sana,kwakweli maisha ni magumu naishi kwa kusaidiwa na ndugu tu sasa hivi  na kibaya zaiid ni kwamba kipindi nafungiwa fedha zangu nyingi nilikuwa nimeweza katika movies, kwaio nikabaki sina kitu kwaio sasa hivi nipo tu nabahatisha maisha .maisha yangu yanategemea sanaa kwa kila kitu.

Kufungiwa kwa Pretty Kindy ilikuwa ni tamko la naibu waziri wa sanaa habari na michezo juliana shonza baada ya kuchunguza wasaniiwanaochapisha  picha za utupu katika mitandao wa kijamii ndio Pretty Kindy na mwenzie Gigy Money wakawa wasanii wa kwanza kupata adhabu hiyo.

mMaagizo ya Naibu Waziri yanakuja baaada ya Mh.Rais kulalamika katika kikao cha jumuiya ya wazazi kuwa vijana hasa wa kike kwa sasa wamekuwa wakikaa uchi sana na kuweka picha katika mitandao ya kijamii ikiacha  sehemu zao kubwa nje.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.