Loading...

Profesa Jay atajavitu ambavyo vilimpendeza katika harusi yake

July 17, 2017 at 17:02
Profesa Jay atajavitu ambavyo vilimpendeza katika harusi yake

Msanii na mbunge kutoka bongo Profesa Jay alifunga pingu za maisha na mpenzi wake Grace – huku akiwavutia wengi kutoka Tanzania.

Sherehe ya harusi yake ilihudhuriwa na wasanii kama Diamond Platnumz, AY na wengi waliotumbuiza wageni na wazazi wa Profesa Jay na Grace.

Hata hivyo hivi karibuni msanii huyu alifunguka kutaja mambo matatu yaliyomvutia Profesa Jay katika harusi yake. Akizungumza na FNL ya EATV Profesa alisema,

“Chakwanza ni support kubwa ya watu wangu wa mtaa, nikaona watu wote wapo pale especially wasanii wenzangu walikuwepo sana sana, wengine walishindwa kuja kwa sababu mbali mbali,”

Aliongeza kusema;

“Pili media ime-play part yake vizuri sana, lakini kikubwa mbacho namshukuru Mwenyenzi Mungu mbele za haki nimejitahidi hata kuungainsha siasa zetu za Tanzania. Viongozi wote waliopata kuongea  walisema huyu jamaa ametuunganisha, watu wa vyama vyote walikuwa pale, watu wa dini zote walikuwepo pale, ni kitu kikubwa namshukuru Mungu,”

Leave a Reply

Be the First to Comment!

avatar
wpDiscuz

in Entertainment
Loading...
I write entertainment stories as well review and critic local music. Apart from my busy schedule you can catch me on social pages by clicking on them below