Proffesa Jay Alalamika Baada ya Jumba Lake La Mamilioni Kuvunjwa

Msanii mkongwe wa Bongo fleva na Mbunge wa Mikumi Joseph Haule au maarufu kama Proffesa Jay amejikuta katika wakati mgumu mno baada nyumba yake aliyokuwa anamiliki iliyopo Mbezi Kimara  kuvunjwa na Tanroads kwa madai ilikuwa imejengwa katika hifadhi ya barabara.

Kwa kupitia ukurasa wake Instagram alifunguka haya;

download latest music    

“Mimi ni mmoja wa wahanga wa zoezi hili la kubomolewa nyumba zetu huko Mbezi Kimara tarehe 29/9/2017,  Jana nikiwa katika majukumu jimboni kwangu Mikumi majira ya saa kumi na mbili jioni, niliitaarifiwa kwamba watu wa Tanroads wakiwa wameambatana na grader mbili na mgari mawili ya polisi yenye askari waliokuwa na silaha mbalimbali za moto walikuwa wanabomoa nyumba yangu. Nimesikitishwa sana jinsi Tanroads wanavyoweza kujichukulia maamuzi bila kujali mhimili muhimu ya mahakama wametoa agizo gani na taratibu zilizotumiwa kubomoa nyumba yangu bila mimi na Tanesco kupewa taarifa saa kumi na mbili jioni na kubomoa huku umeme ukiwa unawaka ni kitendo ambacho kwanza kinahatarisha maisha ya wabomoaji wenyewe maisha ya familia yangu pamoja na majirani”.

Proffesa Jay aliendelea kulaani kitendo hicho alichofanyiwa;

“LIMENISIKITISHA zaidi nasema hivi kwasababu Tanesco wamenigia simu baada ya masaa 24 au zaidi baada ya zoezi hilo na kunitaarifu kuwa wanakuja kukata umeme kabla ya ubomoaji huo pindi nilipo waambia kwamba mbona nyumba imeshabomolewa kabisa na sijaweza kuokoa kitu chochote na hata hiyo meter yenu mnayoulizia mkaitafute kwenye kile kifusi cha nyumba yangu kilichokusanywa kwa pamoja na watu wa Tanroads.Tanesco walishangazwa na kuvunjwa kwa nyumba yangu kwa taratibu zao“.

Proffesa Jay alimalizia kwa kusema

“Lakini naamini kila kitu kinatokea kwa sababu maalumu   nimejifunza kumtegemea na Kumshukuru Mungu kwa kila jambo na hili ni moja ya mitihani ya hapa duniani nimepokea na kumsikiliza Mungu ana mpango gani juu yangu katika familia yangu. Tumelipokea na Naamini tutashinda”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.