Loading...

Q-chillah Afunguka Kukimbiwa na Mke , Kuacha Muziki kwa Sababu ya Madawa.

May 16, 2018 at 09:16
Q-chillah Afunguka Kukimbiwa na Mke , Kuacha Muziki kwa Sababu ya Madawa.

Siku kama moja iliyopita msanii Q-chillah alifumnguka na kutangaza rasmi kuwa ameamua kuach muziki huku akiwa na sema kuwa sababu kubwa ni familia yake ambayo kwa sasa anaona kuwa inamuhitaji sana kuwa nao karibu.

Q-Chillah ambae ameka katika game kwa muda wa miaka 14 katika game la muziki anasema kuwa imefika sehemu inaidi kuwapisha watu wengine kwa sababu kuna watu ambao inad=bidi waendeleze  gurudumu.

Loading...

q-chillah anakiri kuwa ni kwa sababu ya marafiki wabaya ambao alikutana nao na walikuwa hawataki kumuona akiwa katika mafanikio na ndio maana aliweza kuingia katika madawa ya kulevya na hata kupata skendo mbaya katika mitandao ya kijamii.

Q-Chillaha anasema kuwa sababu kubwa ambayo anahisi ilimpelekeka hayo yoet ni baada ya yeye kukosa malezi mazuri kutoka kwa baba na mama yake na ndio maana hata inawezekana kabisa kuwa hakuwa na misingi ya kumfanya asimame katika kile alichokuwa anakiamini sana.

Q-Chillah anasema hakupaswa kuwa msanii hata mara moja zaidi ya kuwa mcheza mpira au daktari kutokana na historia ya wazazi wake, lakini kwa sababu alilelewa na uncles, aunties na grandma ndio maana amekuwa hivyo mpka kufikia hatua ya kujiingiza kwa marafiki wababy waliompeleka katika mada wa ya kulevya.

Q-chillah anasema kuwa swala ya yeye kuingia katika madawa ya kulevya lilimuathiri sana yeye lakini hasa familia yake kutokana na maswali mengi waliokuwa wakikutana nayo ndugu zake , mke wake na hata watoto wake waliokuwa wakienda shule na hii ilimpelekea kutaka kutoka kabisa katika tatizo hilo.

Q-Chillah anasema kuwa mke wake alimkimbia na kumuacha kwa sababu ya kutumia madawa ya kulevya.

 

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…