Q-Chillah Afunguka Kupotea Kwa Siku Tatu Bila Mawasiliano.

Siku chache zilizopita msanii mkongwe wa muziki nchi Q-chillah alisemekana kutoweka nyumbani kwake na ndugu na watu wake wa karibu kushindwa kumfika kimawasilianao hivyo kuwatia wasiwasi watu wake wa karibuni kwa muda wa siku tatu hivyo kudhani kuwa msanii huyo ametekwa na kufanywa vitu vibaya.

Q-chillah amefunguka na kusema kuwa kupotea kwake kwa kutatanisha kulitokana na kukosa mawasiliano sehemu aaliyokuwepo ambapo alikuwa ametoka na rafiki yake kwenda kwenye mazungumzo.

download latest music    

Akizungumza na risasi vibes Q-chillaha anasema kuwa amesikitishwa sana na huzuni aliyowaachia watu wake wa karibu baaada ya kutokupatikana kwake kwa sabab hakutegemea kama itatokea icho kilichotokea kwa sababu ni kitu ambacho hakupanga kufanya hivyo lakini yeye yuko salama wala hakupoatwa na tatizo lolote baya.

nimeumia sana sikujua kama hayo mambo yatakuwa makubwa hivyo,kunarafiki yangu mmoja alikuwa hapa Dar akaniambia kuwa alikuwa na mazungumzo na mimi.

sikumkatalia na tulipanga kuwa tutaenda kufanyia mazungumzo yeti mkoani Morogoro,tukaenda  hadi sehemo moja Morogoro inaitwa Matombo.kufika nikakuta kule kna views nzuri za mimi kuweza kuja kufanya video zangu za mbeleni.basi tukazidi kuzonga lakini sikujua kuwa huko tunakoenda mawasiliano yanazidi kukatika kabisa,simu yangu ikakata netiweki na tayari tulikuwa tulishafika mbali sana.

ilinichukua siku mbili kule , siku ya tatu narudi   lakini simu yangu bado ilikuwa ikisumbua netiweki , nikashughulikia tatizo ili nakuja kuiwasha nakuta meseji nyingi sana  kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki zangu.

Familia ya Q-chillah iliapta wasiwasi kutokana na matukio mengi yanayowatokea wasanii ya kuwa wanatekwa na kwenda pasipojulikana na kuumiza hata wengine kuuwawa.Hata hivyo Q-chillaha anaomba radhi kwa watu wote waliokuwa na hofu ju yake na kuwahakikishia kuwa yeye yuko salama kabisa.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.